March 16, 2016


YANGA

Yanga imeingia kambini katika Hoteli ya Valley View iliyopo Kariakoo jijini Dar kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wake wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya APR ya Rwanda.

Yanga inatarajia kurudiana na APR ya Rwanda Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar huku ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mabao 2-1 ugenini.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro, amesema timu yake hiyo imeweka kambi kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa marudiano dhidi ya APR ambao wanahitaji kushinda.

“Hali ya kikosi kwa ujumla ipo vizuri kuelekea mchezo huo wa marudiano na timu imeshaingia kambini kwa ajili ya maandalizi,” alisema Muro.

Kwa hali ilivyo, Yanga inaonekana kuwa makini kwa kuwa APR bado wana kikosi kizuri na pia kinaweza kushinda ugenini.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV