March 19, 2016


Al Ahly imeimaliza Libolo kwa mabao 2-0 katika mechi kali Waarabu hao wababe wa soka wakiwa nyumbani. Sasa ni Yanga dhidi ya Ahly.

Yanga imeitoa APR kwa mbinde kwa jumla ya mabao 3-2, sasa inakutana tena na Al Ahly waliowatoa katika michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa.

Katika mechi ya leo, Al Ahly ilianza kupata bao lake katika dakika ya 10 Sobhy likadumu hadi mapumziko na kipindi cha pili ikafunga bao la pili kupitia Antui aliyemaliza kazi katika dakika ya 83.

Wakati wanaitoa Yanga, Ahly walionekana kuwa wachovu, kwani walilazimika kuwang’oa Yanga kwa mbinde wakiwa chini ya Kocha Hans van der Pluijm.

Pluijm  aliingoza Yanga kuitwanga Ahly bao 1-0 jijini Dar es Salaam, iliposafiri hadi Alexandria, Yanga ikafungwa bao 1-0. Wakaingia kwenye mikwaju ya penalti, ikang’oka.


Mbuyu Twite na Said Bahanuzi ndiyo waliopoteza penalti kwenye Uwanja wa Jeshi wa jijini Alexandria.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV