May 25, 2016


MPIRA UMEKWISHAAAA-YANGA MABINGWA WAPYA WA KOMBE LA FA

DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
Dk 89 hadi 90, Yanga wanaonekana kucheza taratibu kwa kuwa wameridhika na mabao yao matatu
SUB Dk 88, Yanga wanamtoa Bossou na nafasi yake inachukuliwa na Nadir Haroub Ali

Dk 85 hadi 87 Yanga wanaonekana kutawala mpira kwa kugongeana taratibu
SUB Dk 84, Azam wanamuingiza Shabani Iddi kuchukua nafasi ya Farid Mussa
GOOOOOOOOO Dk 81 Kaseke anaunganisha krosi safi kabisa ya Msuva na kuandika bao la tatu kwa Yanga
Dk 77, Tambwe anatuliza mpira kifuani, anaachia bunduki kali, mpira unaokolewa kwa umahiri mkubwa na Manula na kuwa kona. Inachongwa, inaokolewa
Dk 74 hadi 76, Azam wanaonekana kuutawala sana mpira
Dk 73 Manula anafanya kazi ya ziada kupangua mpira wa kichwa wa Msuva

KADI Dk 72 Gadel Michael analambwa kadi ya njano kwa kumwangusha Msuva
 Dk 71, Juma Abdul peke yake na kipa Aishi Manula, anampa mikononi mwake
Dk 66 hadi 71, Azam FC wanaonekana kutawala zaidi mpira
SUB Dk 65 Yanga wanamtoa Niyonzima na nafasi yake anachukua Twite
KADI Dk 64, Mugiraneza analambwa kadi kwa kumvuta Tambwe

SUB Dk 63 Frank Domayo anaingia kuchukua nafasi ya Mudathir Yahaya upande wa Azam FC
Dk 62, Gadel Michael anajaribu kupiga shuti hapa lakini linakuwa chakula kwa Dida
SUB Dk 57, Haji Mwinyi anaingia kuchukua nafasi ya Joshua aliyeumia
Dk 55, Joshua anatolewa nje baada ya kuumia, inaonekana anapelekwa vyumbani kabisa
Dk 49 hadi 53, mpira unaonekana wa kugongana na kila upande ukionekana kuwa na haraka. Bado timu hazijatulia vizuri licha ya mabao mawili ya haraka katika kipindi cha pili mapema

GOOOOOOO Dk 48, Kavumbagu anaifungia Azam FC bao safi akiunganisha krosi safi ya Singano akitumia kifua kuuukwamisha mpira wavuni
GOOOOOOOOOO Dk 47 Tambwe anafunga bao safi kabisa katikati ya mabeki wa Azam FC akiunganisha krosi maridadi ya Simon Msuva
Dk 46, kipindi cha pili kimeanza kwa kasi huku Azam FC wakiwa wa kwanza kufika katika lango la Yanga
SUB Dk 46, Azam wanamtoa Bocco, nafasi yake inachukuliwa na Kavumbagu

MAPUMZIKO
DAKIKA 2 ZA NYONGEZA
Dk 44, inaonekana Azam FC wanataka kuvizia kufanya shambulizi la kushitukiza, lakini hawajajipanga vema
KADI Dk 42 Singano analambwa kadi ya njano kwa kutaka kumkanyaga kwa makusudi Yondani
Dk 41, Niyonzima anapiga shuti hapa lakini mabeki Azam FC wanaokoa
KADI Dk 40, Aggrey Morrris analambwa kadi ya njano kwa kumwangusha Msuva

Dk 35, nusura Tambwe afunge tena krosi ya Msuva lakini Nyoni anaokoa na kuwa kona. Inachongwa kona safi kabisa, Tambwe anapiga kichwa tena, goal kick
Dk 33, Farid anatoa pasi safi kabisa kwa Bocco ambaye anapiga shuti mtoto kabisa hapa!
Dk 29, Himid aanachia shuti kali kabisa, Dida anapangua na mwamuzi anasema off side, Mudathir aliwahi

Dk 27, krosi safi ya Juma Abdul, Tambwe anaruka na kupiga kichwa safi, goal kick
Dk 25, Farid anaingia vizuri, Juma anatoa na kuwa kona. Inachongwa na Himid, inaokolewa na kuwa kona tena. Inachongwa na Singano, Dida anadaka kwa mbwembwe kabisa
Dk 22, Bocco anajaribu kuingia vizuri kabisa lakini anaanguka mwenyewe na mwamuzi anasema, goal kick
Dk 18 hadi 20 kila timu inaonekana kushambulia kwa zamu lakini hakuna mashambulizi makali
Dk 17, Azam FC wanafanya kosa kubwa kabisa, kipa na mabeki wanajichanganya Tambwe anaruka na kupiga kichwa, bahati kwao kwa kuwa mpira haukulenga lango

Dk 16, mpira unazidi kuchangamka, Juma Abdul anapiga krosi nyingine, hatari kabisa lakini Aishi manula safari hii anatokea na kuiwahi vizuri
Dk 14, Niyonzima anapoteza mpira, Bocco anaupata na kutuliza kifuani, anaachia shuti kali lakini anashindwa kulenga lango
Dk 11 hadi 13, Azam FC wanaonekana kuchankamka wakitaka kurudisha bao hilo la mapema
GOOOOOOOO Dk 9 Tambwe anaruka vizuri na kufunga bao safi kabisa la kichwa akiunganisha krosi ya Juma Abdul
Dk 6 sasa, timu zote zinaonekana kupania na kucheza kwa nguvu sana lakini bado mipira mingi inaishia katikati ya uwanja
Dk 3, Niyonzima ambaye ni nahodha wa Yanga leo, anaonyesha umahiri wake kwa kuwatoka mabeki wa Azam. Wanaokoa na kuwa kona lakini haina manufaa kwa Yanga
Dk 1, Azam wanakuwa wa kwanza kufikisha shambulizi baada ya Farid Mussa kuingia na kupiga shuti lakini Dida anadaka vizuri.

2 COMMENTS:

  1. Hii ndo Yanga bwana. Na mechi hii tumebebwa? 3 - 1?

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV