July 16, 2016


Bao alilofunga mshambuliaji wa KRC Genk, Mbwana Samatta dhidi ya Buducnost Podgorica katika mechi ya kuwania kucheza Europa Cup, limekuwa gumzo.

 Samatta ambaye ni Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania, alifunga bao hilo na kuihakikishia Genk ushindi wa mabao 2-0 ikiwa nyumbani katika mechi ya kwanza wakicheza kwenye Uwanja wao wa Cristal Arena.

Katika dakika ya 79 Samatta alipewa mpira pembeni mwa uwanja huku ukionekana kama hauna madhara, akageuka nao kwa haraka na kukimbia kama hatua nje, huku ikionekana kama atatoa upasi, umbali kama wa mita 25 hivi, akaachia mkwaju mkali na kufunga bao safi kabisa.


Katika mitandao mbalimbali ya kijamii, bao hilo limekuwa gumzo huku mashabiki wa soka wa Genk na wale wa Tanzania wakijadili ubora wake.

Bao hilo limekuwa muhimu kwa Genk kwa kuwa inajiwekea nafasi nzuri kabla ya mechi ya marudiano. Lakini nimemtangaza zaidi Samatta kutokana na ubora wake.

Timu hizo zitarudiana Julai 21, 2016 kwenye Uwanja wa City jijini Podgorica ambapo Genk itakuwa ugenini.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV