November 20, 2016

Unaweza kusema hawa wazee wana lao jambo. Jose Mourinho na Arsene Wenger wanaonekana kweli hawaivi chungu kimoja.

Baada ya mechi ya Ligi Kuu England kati ya Manchester United dhidi ya Arsenal, makocha hao walipeana mkono kwa staili ambayo inaonyesha ilimradi.

Mara baada ya mechi walikutana na kupeana mkono kama sehemu ya kutimiza wajibu lakini hakuna aliyemtazama mwenzake usoni wala kuzungumza.

Mechi hiyo iliisha kwa sare ya bao 1-1, Arsenal wakisawazisha mwishoni kupitia Mfaransa Olvier Giroud aliyeingia kipindi cha pili.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV