January 13, 2017Azam FC imefunga Simba kwa bao 1-0 katika mechi ya fainali ya Kombe la Mapinduzi kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar.

Kwa Ushindi huo, Azam FC wanakuwa mabingwa Mapinduzi 2017 lakini wanaweka rekodi ya kubeba kombe hilo bila ya kupoteza mchezo wala kufungwa hata bao moja.


Azam FC imeishinda Simba katika mchezo safi na kufanikiwa kubeba kombe hilo mara tatu sawa na Simba ambayo pia imewahi kulibeba mara Simba huku mabingwa wengine kama Yanga na Mtibwa Sugar wakiwa wamewahi kulibeba kombe hilo mara moja tu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV