January 14, 2017



Pamoja na kupoteza mechi ya fainali dhidi ya Azam FC na kuukosa ubingwa, Bosi Msaidizi wa benchi la ufundi la Simba, Jackson Mayanja ameibuka na kusema kuwa, michuano ya Kombe la Mapinduzi imewasaidia kuwajenga na kuwapatia kikosi bora kitakachopambana kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

Michuano ya Kombe la Mapinduzi imefikia tamati jana kwa kuzikutanisha Simba na Azam ambapo Azam FC iliibuka na ushindi wa bao 1-0 na kumaliza mashindano bila ya kufungwa mechi wala bao hata moja.


Mayanja alisema michuano hiyo imewasaidia katika kukiimarisha kikosi chao kwa lengo la kufanikisha mikakati yao ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu.

“Tatizo letu kubwa katika kikosi chetu ni safu ya ushambuliaji hasa katika suala zima la umaliziaji, hivyo tumetumia muda huu kukijenga vyema kwa kikosi kuhakikisha tunafanikiwa kupata mabao ya mapema.

“Naamini iwapo tutapata mabao ya harakaharaka ambayo ndiyo yatakayotuweka katika nafasi nzuri zaidi ya ushindi, michuano hii imesaidia kujenga kikosi chetu na kubaini makosa mbalimbali.

“Mwisho wa siku tutaweza kufanikiwa kutwaa ubingwa hivyo naamini kila mchezaji atakuwa ametoka na nguvu mpya katika michuano hii.

“Mara baada ya kumaliza michuano hii akili zetu zote tunazielekeza kwenye ligi ambapo lengo letu kubwa ni kuona tunafanikiwa kutwaa ubingwa,” alisema Mayanja.


1 COMMENTS:

  1. Kwa forward line ipi??....Ushauri wangu wampe nafasi Ibrahim Ajib kucheza kama mshambuliaji wa kati huku wakimpunguzia majukumu ya kushuka chini kutafuta mipira na kumpa nafasi ya kupiga mipira yote iliyokufa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic