January 15, 2017Nahodha wa Simba, Jonas Mkude amesema baada ya kulikosa Kombe la Mapinduzi, hawatafanya mchezo katika Ligi Kuu Bara.

Simba itarejea kwenye Ligi Kuu Bara kwa kucheza na Mtibwa Sugar ikiwa ugenini Morogoro, Jumatano.

Mkude amesema michuano ya Mapinduzi ambayo walifika fainali na kupoteza dhidi ya Azam FC kwa bao 1-0, imepita na sasa ni ligi kuu,

“Ni michuano mizuri kwetu, tumejifunza na kupata kitu kizuri kwa kweli. Mpira hauwezi kushinda kila siku, lazima kuna siku mambo yataenda tofauti.

“Uliona tulivyojitahidi, lakini imeshindikana. Sasa tunarudisha nguvu zetu ligi kuu,” alisema.


Simba ndiyo vinara wa Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 44 wakifuatiwa na mabingwa watetezi Yanga wenye 40.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV