January 19, 2017
Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Lindi, imemhukumu Selemani Mathew kwenda jela miezi nane (bila ya faini).

Mathew ambaye alikuwa mgombea Ubunge wa Jimbo la Mtama kupitia CCM kabla ya kuhamia Chadema, amepatikana na hatia ya kufanya mkutano au kufanya mikusanyiko bila ya kibali.


Mathew aliwahi kuichezea Yanga, Simba na pia amewahi kuwa muandaaji wa mechi za wakongwe wa Yanga na Simba.

Mathew ni mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Lindi. Mwingine ambaye amehukumiwa pamoja naye ni katibu wa Chadema Tawi la Nyamangala Ismail Kupilila.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV