January 16, 2017


Togo imeanza michuano ya Kombe la Mataifa Afrika nchini Gabon kwa sare ya bila bao.

Beki wa Yanga ambaye anakipiga katika kikosi cha Togo alikuwa kati ya wachezaji wa akiba kwa dakika zote tisini.

Bossou hakupata nafasi ya kucheza licha ya Kocha wa Togo, Claude Le Roy ‘Mchawi Mweupe”  kufanya mabadiliko yote matatu yanayotakiwa katika mechi moja.


Mabadiliko ya kwanza yalikuwa katika dakika ya 83 alipotoka Kodjo Laba na kuingizwa Serge Akakpo, dakika ya 89 akatoka Mathieu Dossevi nafasi yake ikachukuliwa na Komlan Agbegniadan na mabadiliko ya mwisho, Emmanuel Adebayor akatoka dakika ya 89 na Razak Boukar akachukua nafasi yake.

Mechi hiyo ilikuwa ni ya Kundi C na mechi inayofuata baadaye ni kati ya Morocco dhidi ya DR Congo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV