January 15, 2017
Kiungo wa zamani wa Simba, Abdulhalim Humud ameibuka na kusema alianza kupoteza mwelekeo wakati akiwa Simba.


Humud ambaye msimu uliopita, alikipiga Coastal Union ambayo iliteremka daraja hadi la kwanza, amesema hajui kilichomtokea Simba.

“Sitaki kuisema Simba vibaya, lakini nilianza kupoteza mwelekeo nikiwa katika Simba. Sijui kwa kweli kilichotokea,” alisema.

Hata hivyo, video yake hiyo akifanya mahojiano na Times FM imezua gumzo kwenye mitandao mingi.


Wako wanaomuunga mkono alichosema huku wengi wakimpiga kwamba alilewa sifa na kutanguliza majivuno hali iliyochangia kushindwa kuendelea kufanya vema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV