January 21, 2017
Huku beki wa Simba, Juuko Murshid akiwa anaongoza ulinzi wa kikosi cha Uganda, imeshindwa kuhimili mawimbi ya Misri na kuchapwa kwa bao 1-0 katika michuano ya Afcon.

Mechi hiyo ya kuvutia yenye kasi, imeisha kwa Misri na ushindi huo ambao ulipatikana dakika moja kabla ya mpira kwisha. Sasa Uganda imeaga michuano hiyo huku ikisubiri mchezo mmoja dhidi ya Mali.

Abdallah Al Said alifunga bao hilo dakika ya 99 baada ya Misri kufanya shambulizi kali na Mohammed Salah kama anapiga shuri kali, badala yake akatoa pasi safi iliyozaa bao hilo.Uganda walijitahidi kushambulia na kwa ujumla walicheza vizuri wakionyesha soka la ushindani.

Hata hivyo, mara kadhaa walipoteza nafasi huku kipa wao, Denis Onyango akionyesha umahiri mkubwa kabla ya kushindwa kuhimili shuti hilo la Al Said uliopita katikati ya miguu yake dakika moja kabla ya mpira kwisha.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV