January 19, 2017


Kiungo mshambuliaji wa Simba, Shiza Kichuya amefikisha siku 78 bila ya kufunga hata mechi moja.

Mara ya mwisho, Kichuya aliifungia Simba kwa penalti ilipoivaa Stand United Novemba 2.

Lakini jana, Kichuya ameichezea Simba mechi ya sita ikiwa ni dakika ya 540 bila ya kufunga hata bao moja.


Kwa sasa Kichuya ana mabao tisa ya kufunga akiwa anaongoza msimamo wa wafungaji sawa na Simon Msuva na Amissi Tambwe anayshikilia tuzo ya mfungaji bora.

Mwanzoni mwa ligi, Kichuya ambaye amejiunga na Simba msimu huu akitokea Mtibwa Sugar alionekana ni hatari huku akifunga mfululizo.

2 COMMENTS:

  1. Jukumu la Kwanza kabisa la Kichuya sio ufungaji... .maneno yenu waandishi na uchambuzi unaolalia upande mmoja wala si sahihi. Pili unamuhesabia Kichuya dakika pasipo kukumbuka michezo kadhaa hakumaliza aliitwa nje kupisha wengine. Toa hizo dakika kisha tunza kumbukumbu zako vema.

    Kichuya pia anaweza kurudi kwenye foam yake kama atapata msaada wa kisaikolojia sio namna hii na mabango haya. ENDELEA MBELE SHIZA RAMADHANI KICHUYA tafakari mchezo na kuisaidia Simba kupata matokeo na si maneno kama haya.SIMBA KWANZA

    ReplyDelete
  2. Jukumu la Kwanza kabisa la Kichuya sio ufungaji... .maneno yenu waandishi na uchambuzi unaolalia upande mmoja wala si sahihi. Pili unamuhesabia Kichuya dakika pasipo kukumbuka michezo kadhaa hakumaliza aliitwa nje kupisha wengine. Toa hizo dakika kisha tunza kumbukumbu zako vema.

    Kichuya pia anaweza kurudi kwenye foam yake kama atapata msaada wa kisaikolojia sio namna hii na mabango haya. ENDELEA MBELE SHIZA RAMADHANI KICHUYA tafakari mchezo na kuisaidia Simba kupata matokeo na si maneno kama haya.SIMBA KWANZA

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV