January 18, 2017MPIRA UMEKWISHAAA

DAKIKA 4 ZA NYONGEZA

Dk 89, Mtibwa wanafanya kazi ziada kuokoa mpira wa faulo
Dk 86, Kipa Mohammed anafanya kazi ya ziada na kuugusa mpira uliokuwa unajaa wavuni, kona. Simba wanachonga lakini haina madhara
SUB 85, Mtibwa Sugar wanamuingiza Hussein Javu kuchukua nafasi ya Jaffar Salum
SUB Dk 83 Simba wanamtoa Kichuya, nafasi yake inachukuliwa na Jamal Simba Mnyate 
Dk 81, nafasi nzuri kwa Mtibwa, mabeki wa Simba wanagongana na mpira unamkuta Friday, lakini anapinga shuti matege....hakuna kitu


Dk 79, Mandawa tena, anaachia mkwaju mkali lakini anapaisha juuu
SUB Dk 77, Barnabas anaingia Kelvin Friday
SUB Dk 75, Simba wanamtoa Kazimoto na nafasi yake inachukuliwa na Pastroy Athanas
Dk 73, Ajibu anafanya kazi ya kugeuka na kuachia shuti hapa, Said Mohammed anaokoa na kuwa kona ambayo haina madhara
Dk 72, Mandawa amegeuka anapiga shuti kali kabisa hapa lakini Agyei anadaka kwa ufundi mkubwa kabisa
Dk 70, Banda anaachia mkwaju mkali kabisa hapa lakini unamgnga beki Mtibwa na kuwa kona
Dk 68, Kichuya anawachambua mabeki wa Mtibwa lakini Shomari anatoa na kuwa kona, inachongwa na kuokolewa
Dk  65 Baba Ubaya anagongana na Hamad Juma na wote wako chini wanatibiwa


KADI Dk 64, Issa Rashid "Baba Ubaya" analambwa kadi yah njano kwa kumuangusha Kazimoto
Dk 59, Kichuya anamtoka Baba Ubaya, krosi safi kabisa lakini Mbonde anaruka na kupiga kichwa safi kabisa
Dk 57, Liuzio anamzidi mbio Henry lakini anashindwa kuudhibiti mpira kutokana na uwanja kuwa mbovi
Dk 54, Simba wanamuingiza Ajibu kuchukua nafasi ya Mavugo
Dk 50, mpira bado unakuwa ni wa kubutua zaidi lakini safu ya ulinzi ya Simba wanapaswa kuwa makini hasa pembeni
DK 45,Mtibwa wanaanza kwa kasi, krosi matata ya barnabas nakuwa kona


MAPUMZIKO
Dk 44, MAvungo anajaribu kuingia tena lakini Henry Joseph anaondosha hatari
Dk 41 Mavugo anageuka na kuachia fataki hapa, linatoka kidogo juu la lango la Mtibwa
Dk 37, Luizio na Kotei wanafanya kazi nzuri hapa, wanagongeana vizuri lakini shuti la Mavugo linashindwa kulenga
Dk 36, ladha ya mpira ni butuabutua zaidi kuliko pasi za uhakika
Dk 31 Kotei anafanya anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira miguuni mwa Chanongo akiwa anakaribia kuachia fataki karibu na lango la Simba. Inakuwa kona, inachongwa na Issa Rashid lakini Simba wanaokoa


Dk 28, Luizio anamtoka Ali Shomari, anapiga krosi safi kwa Mavugo akiwa yeye na kipa Mohammed lakini anashindwa kufunga
Dk 20, hakika mpira hauna mvuto sana. Mtibwa Sugar wanapata kona, inachongwa vizuri na Mandawa anapiga kichwa safi kabisa, lakini Agyei anadaka vizuriDk 15 Kotei mita 28 anaachia shuti kali lakini Said Mohammed anadaka vizuri kabisa
Dk 14, Mtibwa Sugar wanafanya shambulizi kali hapa, lakini Simba wanaokoa na kuwa kona. anaichonga Baba Ubaya lakini Simba wanaokoa vizuri


Dk 11 sasa, mechi ina presha kubwa. Lakini zaidi mpira unachezwa katikati na uwanja unaendelea kuonekana tatizo katika umiliki wa mpira
Dk 6, Simba wanapata kona, anaichonga hapa Kichuya lakini ni kona hovyoooo
Dk 4 mpira safi wa krosi wa Hamad Juma lakini unakosa mtu, Mtibwa wanaokoa
Dk 1, mpira umeanza lakini ikionekana kuanza kwa kubutua. Mtibwa wanapata faulo si mbali na lango la Simba

KIKOSI MTIBWA:
1-Said Mohamed
2-Ally Shomary
3-Issa Rashid
4-Henry Joseph
5-Salim Mbonde
6-Shaban Nditi
7-Haruna Chanongo
8-Ally Makarani
9-Rashid Mandawa
10-Jaffary Salum
11-Vicent Barnabas

SUB
-Benedict Tinoko
-Rogers Gabriel
-Kassian Ponera
-Dickson Daudi
-Ibrahim Rajabu Jeba
-Kelvin Friday

-Hussen Javu


KIKOSI SIMBA:
1. Daniel Agyei, 
2. Hamad Juma,
3. Mohamed Zimbwe
4. Abdi Banda
5. Method Mwanjale,
6. Jonas Mkude
7. Shiza Kichuya
8. James Kotei
9. Laudit Mavugo
10 Juma Liuzio
11. Mwinyi Kazimoto

Sub…
Peter Manyika
Novatus Lufunga
Jamal Mnyate
Pastory Athanas
Mzamiru Yassin
Ibrahim Ajibu

2 COMMENTS:

  1. Apandacho Simba ndicho atakachovuna....Makocha mmuamini Ajib na mumpe muda wa kutosha wa kucheza na mumjaribu kumchezesha na Pastory na Luizio kwa pamoja....sio hii panga pangua ya kila siku mpaka leo Simba haina Best combination hapo mbele. Pili uwezo wa Mwl nafikiri umefikia kikomo

    ReplyDelete
  2. Labda wadau wengine mnisaidie kuniambia mbinu au mfumo wa kiuchezaji wa kushambulia kwa kutengeneza nafasi na kufunga magoli ambao unaonekana umetengenezwa na Mwalimu. Nadiriki kusema magoli yote ya Simba yamekuwa ni ya juhudi binafsi za wachezaji,makosa ya team pinzani,kudra za Mwenyezi Mungu na WALA SIO YA KIMFUMO.

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV