January 15, 2017


Wachezaji wa kikosi cha Majimaji wameonekana wakinywa chai na chapati huku wakiwa ni wenye furaha kabla ya mechi yao dhidi ya Yanga keshokutwa Jumanne.

Majimaji wanaisubiri Yanga katika mechi ya Ligi Kuu Bara ambayo itakuwa ni ya kwanza ya Yanga wakirejea katika ligi hiyo baada ya michuano ya Mapinduzi.

Wakati Yanga wakitaka kushinda mechi hiyo, Majimaji pia ushindi utakuwa muhimu kwao kwa kuwa wako katika nafasi ya 14 wakiwa na pointi 17 na si sehemu salama kwao hata kidogo.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV