January 24, 2017





Na Haji S Manara

Kuna kurogwa na kujiroga, kuna kufa na kujiua pia kulia na kuliliwa. Sisi Watanzania hakika tupo katika fungu la pili, fungu la kukosa , fungu mzigo, tunajiroga, tunajiua na tunaliliwa.

Hakika hatujui twataka nini, hatujui malengo yetu, lakini kubwa hatujui hata tutokapo wala tuendako, na leo naandika kitu kidogo tu kinachotushindwa kwenye soka letu, RATIBA!!

 Wakati wenzetu wanazungumzia  changamoto nzito na kubwa ktk maendeleo yao ya mchezo murua zaid duniani wa soka, Watanzania tunahangaika namna ya kupanga ratiba ya mechi zetu za ligi yetu na Kombe la Shirikisho, ratiba inayobadilishwa Kama nguo, tena mvaaji mwenyewe ni mbunifu wa mavazi au mwanamitindo, ambae huvaa nguo tano kwa siku.

Siku za nyuma niliwahi kuwaambia Clouds FM kuwa, iwapo ratiba ya Ligi Kuu nchini isipopanguliwa ntatembea bila shati toka Mtaa Msimbazi hadi zilipo ofisi za TFF pale Karume Stadium.

Nilidhani Kwa kusena vile walau TFF na bodi ya Ligi wataona haya na kuhakikisha ratiba ya Ligi kuu haitabadilishwa tena, kumbe ndio kwanza wakubwa wameweka gundi masikioni, toka wakati ule ratiba ishafumuliwa Mara tatu, na leo hii imebadilishwa tena, Kwa kisinguzio kile kile, eti ratiba za Caf na za ligi zimeingiliana. 

 Ninajiuliza iwapo ratiba ya Ligi yetu ni muhali kuipanga,vipi kuhusu programu nyingine za maendeleo? 

Itakuwaje kuhusu timu yetu ya taifa juu ya ndoto zetu za mchana wa jua kali? vipi kuhusiana na zile programu hewa za soka la vijana, watoto na wanawake?

 Hakika kwetu hayo ni sawa na bahari ya Mediterranean au bahari kuu ya hadithi za Alfu Leila uleila, hatuwezi ratiba tutaweza kwenda Afcon 2019? Hatuwezi kupanga ratiba tutaweza kuwa na mipango madhubuti ya kuendeleza mchezo huu ambao yatajwa watu bilioni tatu duniani kote wanaushabikia? 

Kama tumerogwa aliyeturoga Kafa, hatuponi hadi kiyama , tutakapokutana nae mchawi wetu. 


Nimalizie Kwa kuwapa mtihani mwingine TFF na bodi ya Ligi, iwapo Kama ratiba yao ya Ligi kuu na Kombe la shirikisho haitabadilishwa kuanzia sasa hadi mwisho wa msimu, ntamposa mlimbwende Wema Sepetu, na akikubali ntamuoa, akikataa ntatembea na boxer toka nyumbani kwangu hadi TFF.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic