January 18, 2017



Wakiwa wanaingia uwanjani leo kuvaana na Simba, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru ametamba hawawaogopi mastaa wa timu huku akitamba kuwashushia kipigo.

Timu hizo, zinatarajiwa kuvaana leo kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Mtibwa katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam ilichezea kipigo cha mabao 2-0 yakifungwa Ibrahim Ajib na Laudit Mavugo.

Kifaru alisema wanaiheshimu Simba, lakini wala hawawaogopi kutokana na ubora wa kikosi walichonacho.

Kifaru alisema, nusu ya wachezaji wanaounda timu hiyo wanawafahamu ambao walitokea Mtibwa ambao waliwalea wenyewe, hivyo haoni sababu ya kuwaogopa.

Baadhi ya wachezaji hao ni Shiza Kichuya, Mohamed Ibrahim na Mzamiru Yassin.

“Tunafahamu Simba ina mastaa wengi wanaounda timu hiyo, kati ya hao baadhi tunawafahamu ambao wametokea kwenye mikono yetu hapa Mtibwa, hivyo hatuoni sababu ya kuwaogopa.

“Hivyo hatuwaogopi hata kidogo na tumepanga kuwafunga kwenye mechi hiyo licha ya kuwepo ushindani mkubwa katika mchezo huo.

“Kikubwa tunataka pointi tatu muhimu zitakazotuweka katika nafasi nzuri katika msimamo wa ligi kuu,” alisema Kifaru.

Mtibwa wapo katika nafasi ya nne wakiwa na pointi 30 huku Simba wakiwa kileleni kwenye Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi  44.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic