January 16, 2017
Mshambuliaji mpya mwenye kasi wa Yanga, Emmanuel Martin amelazimika kutosafiri na kikosi cha timu hiyo kwenda mjini Songea kuivaa Majimaji katika mechi ya Ligi Kuu Bara, kesho.

Martin amepata msiba wa kufiwa na mdogo wake, hivyo kulazimika kubaki ili amalize suala hilo la kifamilia.

Kocha Msaidizi wa Yanga, amesema Martin amebaki huku akiungana na wachezaji wengine ambao pia wamebaki jijini Dar es Salaam.

“Pia kuna wale walio majeruhi kama (Donald) Ngoma na (Obey) Chirwa ambao ni majeruhi,” alisema Mwambusi.


Mwambusi alisema wachezaji wengine wako fiti na tayari wamewasili salama wakifanya maandalizi ya mwisho kabla ya mechi hiyo ya kesho.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV