January 20, 2017Mashabiki wa Simba sasa wanataka klabu hiyo mara moja ichangamke na kumpata mshambuliaji Emmanuel Okwi.

Okwi raia wa Uganda amevunja mkataba na klabu ya 
 SønderjyskE ya nchini Denmark.

Uamuzi huo umetokana na yeye kukosa namba ya kudumu katika kikosi cha kwanza na mashabiki Simba wameona ni wakati mwafaka wa kumnasa.

Kupitia maoni ya salehkubwa@gmail.com, mashabiki hao wameutaka uongozi wa Simba kumchangamgia Okwi mapema.

“Tumeona kwenye gazeti la Championi uongozi ukimkaribisha nyumbani msimu ujao. Lakini vizuri mipango ianze sasa,” alisema Mjarubi Hamisi wa Biharamulo.

“Uongozi ukutane na Okwi mapema kabisa, tunamhitaji sana,” alisema Zainabu Kamuntu ‘Mama Rajab’ wa Tanga.

Wakati John Tamba wa Kigoma, alisema: “Sidhani kama itakuwa vizuri kusubiri wakati Okwi ni mchezaji huru. Simba wampe mkataba maana mwezi wa tano si mbali.”

Mashabiki wengi wa Simba walisema wamechoshwa na mateso hasa kuporomoka kwa Simba hivyo mtu anayeweza kubadilisha hali ya hewa, ndiye rafiki yao.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV