January 15, 2017

Kiungo na beki wa zamani wa Yanga, Mbuyu Twite sasa ni rasmi mchezaji wa Fanja baada ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja.

Twite raia wa DR Congo, amesaini mkataba huo na kukabidhiwa jezi yake. Hii ilikuwa ni baada ya mazungumzo ya siku kadhaa.

Twite aliondoka Yanga baada ya klabu hiyo kuitaka nafasi yake ili imsajili Justice Zulu, kiungo kutoka Zambia.

Timu kadhaa za Ligi Kuu Bara zilionekana kumuwania Twite, lakini mwisho aliamua kutua Fanja ya Oman ambayo sasa imemsajili na ameanza kuitumikia.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV