January 21, 2017


Klabu ya Djurgårdens IF ya Sweden imemuuza mshambuliaji wake Mkenya, Michael Olunga kwa dial million 40 (Sh bilioni 88) nchini China.

Olunga aliyekuwa mshambuliaji nyota wa Gor Mahia ya Kenya aliyewahi kuzitesa timu za Tanzania, amejiunga na Guizhou Zhicheng Hengfeng kwa dau hilo nono.


Olunga mwenye umri wa miaka 22, alijiunga na Djurgårdens IF msimu mmoja na nusu uliopita akitokea Gor Mahia.

Kwa mujibu wa Sport Express anatarajia kusaini katika timu hiyo hive karibuni na masuala ya kusaini yatafanyika lakini makubaliano yameishafikiwa.


Wakala wake amesema mauzo ya Olunga yatashikilia rekodi ya mauzo ya ligi ya Sweden maarufu kama Allsvenskankwa muda mrefu sana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV