January 13, 2017

MATUMLA

Jumla ya mapambano saba ya ngumi za kulipwa nchini yamepangwa kufanyika jijini Dar es Salaam, Februari 5, mwaka huu.

Bondia Mohammed Matumla 'Snake Boy Jr' atazichapa na Mfaume Mfaume katika pambano la raundi 10 uzito wa Light kuwania ubingwa wa taifa wa TPBC kwenye Uwanja wa Ndani wa Taifa.

Mratibu wa mapambano hayo kutoka Kampuni ya Sadick & Co Ltd, Chase Masanja alisema kuwa siku hiyo pia kutapigwa pambano la kimataifa.

"Katika mapambano hayo, Ramadhan Shauri atazichapa na Meshack Mwankemwa pambano la kuwania mikanda miwili ambao ni wa TPBC na ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati, pambano hili litakuwa la raundi 10 la uzani wa Walter," alisema Masanja.

Mapambano mengine ya siku hiyo, Ibrahim Class atazichapa na Amos Mwamakula, Twalibu Tuwa atazichapa na Said Chino wakati Iddi Mkwela akitoana jasho na Manyi Issa.


Pambano lingine, Ibrahim Maokola atapambana na Zumba Kukwe wakati Haidari Machanjo akitoana jasho Swedi Mohamed.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV