January 26, 2017


Kiungo Mohammed Ibrahim amerejesha matumaini ya Wanasimba.

Ibahim maarufu kama Mo anaonekana kuwa vizuri katika siku zote tatu ambazo Simba wamefanya mazoezi yeye akiwa ndani.

Maana yake, suala la kucheza au la katika mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam FC keshokutwa Jumamosi linabaki kwa Kocha Joseph Marion Omog.


Omog raia wa Cameroon ndiye mwenye nafasi ya kuamua, Mo aliyeumia mara ya mwisho katika mechi ya fainali ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Azam FC, arejee na kuanza wakati wa kuivaa Azam tena au aingie baadaye. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV