January 26, 2017


Kocha Aristica Cioaba ameanza taratibu kuingiza mbinu zake katika kikosi cha Azam FC.

Cioaba raia wa Romania, ameanza kufanya mazoezi na kikosi chake kujiandaa na mechi dhidi ya Simba.

Maandalizi yake yanalenga kutoingiza mambo mengi kwa wakati mmoja.

“Kocha katuambia hataingiza vitu vingi sana hadi kutichanganya lakini mazoezi yake ni mazuri na maandalizi yanakwenda poa.


“Kweli tuna matumaini ya kufanya vizuri katika mechi dhidi ya Simba,” alisema mmoja wa wachezaji wa Azam FC akizungumza na SALEHJEMBE.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV