January 21, 2017Mshambuliaji wa African Sports, Ayoub Lyanga amejiunga na Zanaco ya Zambia.

Lyanga amesajiliwa na timu hiyo kwa mkopo hali ambayo itampa nafasi ya kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Lyanga hakuwa mchezaji maarufu sana nchini ingawa imeelezwa kwamba ana uwezo mkubwa wa soka.

Meneja maarufu katika masuala ya soka nchini, Jamal Kisongo amethibitisha Mtanzania huyo kupata nafasi ya kuichezea Zanaco akitokea African Sports inayocheza Ligi Daraja la Kwanza.

“Kweli kabisa kijana Lyanga amejiunga na Zesco ya Zambia kwa mkopo,” alisema Kisongo.

“Naweza kukuambia kama ataendelea kuwa makini na kuendelea kupambana, basi hakuna kinachoweza kumzuia kufanya vizuri.

“Zanaco ni timu kubwa na inawezekana kabisa itasaidia kumtangaza kama atapata nafasi lakini huyu kijana ninaamini atakuwa hazina kubwa kwa Tanzania. Sipendi niseme mambo mengi ila tusubiri,” aliongeza.

Kisongo ndiye meneja wa nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta lakini ndiye meneja wa mshambuliaji mwingine nyota nchini, Thomas Ulimwengu.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV