January 25, 2017


Nawaomba radhi wasomaji wote wa blog hii namba moja kwa sasa ya michezo.

Kumekuwa na matatizo makubwa ya upatikanaji wa blog hii, hali ambayo imetokana na wavamizi wa mtandao kutengeneza virusi vinavyosababisha usumbufu mkubwa kwa wasomaji wakiwatisha kuwa ukiifungua blog hii, kompyuta au simu yako itapata matatizo.

Hali hiyo inaendelea kufanyiwa kazi na wataalamu mbalimbali wakiwemo wale wa Google ambao wamejua kinachofanyika. (Nashukuru Google, pia watu wa IT ambao wamekuwa wakinisaidia kuweka mambo sawa).

Imani yangu, mambo yatakaa vizuri kuanzia leo au kesho.

Nawaomba radii kwa usumbufu wowote uliojitokeza kwenu na ambao utaendelea kujitokeza.

Kawaida washambulizi hao, huangalia blog zinazosomwa zaidi na kufanya hivyo. Lakini naamini mchango wenu umekuwa mkubwa hadi umewafanya kusikia wivu, lakini juhudi zetu, zitazaa matunda na muendelee kufaidi habari murua za kispoti na burudani kidogo.

Kwa mara nyingine, natoa shukurani kwenu na kuwaomba muendelee kuwa wavumilivu wakati kazi ya marekebisho ikiendelea.

Ahsante

SALEH ALLY

CEO, Founder and Owner of SALEHJEMBE BLOG

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic