January 19, 2017Mashabiki Simba wakata tamaa na Simba wamekata tamaa baada ya timu yao kutoka sare na Mtibwa Sugar.

Mtibwa Sugar iliishikilia Simba kwa sare ya bila mabao katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, jana.

Sare dhidi ya Mtibwa Sugar, Simba imefikisha pointi 45 huku Yanga ikiwa na 43, tofauti ya pointi mbili tu.

Mashabiki wa Simba waliotuma maoni kwenye email ya salehkubwa@gmail.com wamesema, wanaanza kuingiwa hofu ya ubingwa.

“Mwenendo si mzuri, tunaanza kukata tamaa,” alisema Saidi Mohammed Jumaa.

“Mimi naingiwa hofu sana, labda kama tutawafunga Azam, tutarejea tena,” alisema Thomas Ngailo wa Morogoro.

“Kipindi cha hofu kimeanza, sipendi kabisa kufikia hapo,” alisema Rehema Hassan kutoka Mwanza.

Mashabiki 112 waliotuma maoni baada ya sare dhidi ya Mtibwa, 78 wamezungumzia hofu ya kikosi chao huku wakisisitiza wachezaji hawajitumi sana hasa wale wa mbele.

Wako waliotaka kuona Mo Ibrahim anapona mapema na kuongeza nguvu lakini wengi wakasema Juma Liuzio hana msaidizi mbele kwa kuwa anajituma sana lakini wenzake wanaonekana kutokuwa na nguvu ya msaada.


2 COMMENTS:

  1. Hayo ni matokeo ya mchezo,na matarajio ya ubingwa bado yapo palepale.cha muhimimu NI kwa wachezaji kujituma zaidi na mshikamano miongoni mwa viongozi ,wanachama na mashabiki

    ReplyDelete
  2. Hakuna shaka ubingwa uko palepale kwani huko mbele tuna point 3 kutoka kwa 4G

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV