January 18, 2017



 Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili inayoendeshwa na Kampuni ya Global Publishers, wachapishaji wa Magazeti ya Uwazi, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Amani, Risasi na Championi, imezinduliwa rasmi leo kwenye ofisi za Global Publishers, Bamaga- Mwenge jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa  ni Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji na Sheria wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, James Mbalwe.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Global Publishers, Eric Shigongo alisema wameamua kutoa nyumba kama sehemu ya kurudisha wanachokipata kutoka kwa wasomaji na kuwahakikishia kwamba, mchakato mzima huendeshwa kwa umakini, haki na kuzingatia sheria kwa hiyo watu wasiwe na wasiwasi kwamba mshindi atapendelewa.






“Niwahakikishie wasomaji na Watanzania wote kwamba shindano hili lipo ‘fair’ kabisa na maombi yangu ni kwamba kweli nyumba iende kwa mtu anayeihitaji, kama mjuavyo kujenga nyumba Dar es Salaam ni ghali sana na watu wengi wanapenda kuishi Dar es Salaam.


“Awamu hii tumeyafanyia kazi mapungufu yote yaliyotokea kwenye shinda nyumba iliyopita, nyumba imeboreshwa na ipo karibu na barabara, pia samani zote za ndani zimeboreshwa pamoja na mfumo mzima wa ukusanyaji wa kuponi ambapo utamfikia msomaji karibu zaidi sehemu yoyote alipo nchini,” alisema.







Kwa upande wa mgeni rasmi, aliwahakikishia washiriki wote kwamba amekuwa akifanya kazi na Global Publishers na ana uhakika kuwa huwa wanazingatia sheria na ndiyo maana wamewapa kibali cha kuendesha shindano hilo.

“Nimefanya kazi kwa muda mrefu na Global Publishers, huwa hakuna kupanga matokeo wala upendeleo, anayeshinda anakuwa ni yule kweli aliyestahili, nawasihi watu wote washiriki kwa sababu shindano limefuata taratibu zote za kisheria,” alisema.

Kwa upande wa Meneja Mkuu wa Global Publishers, aliwataka watu wengi washiriki kwa sababu yeyote anaweza kuibuka mshindi na kueleza kuwa namna ya kushiriki kuwania nyuumba hiyo iliyopo Bunju, Dar, mshiriki anatakiwa kununua magazeti la Global Publishers, kukata kuponi iliyopo ukurasa wa pili na kuijaza kisha kuikusanya kwa wakala aliye karibu naye nchi nzima au kwenye ofisi za Global Publishers, Bamaga- Mwenge jijini Dar.










0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic