January 16, 2017Kikosi cha Simba kiko tayari kwa ajili ya mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar, keshokutwa.

Meneja wa Simba, Mussa Hassan Mgosi, ameiambia SALEHJEMBE kuwa wanajua michuano ya Mapinduzi, imepita sasa ni Ligi Kuu Bara.

“Tulifika fainali katika Mapinduzi, hatukuchukua kombe. Lakini tunajua sasa kazi iliyo mbele yetu ni ipi.

“Tunachoshukuru wachezaji wanaelewa kabisa tumetoka wapi, tunapokwenda na tunataka nini.

“Wako tayari kwa ajili ya kupambana na tunaendelea kukumbushana kwa kuwa hili ni jambo la kuendelea kukumbusha,” alisema.

Mgosi aliyeichezea Simba kwa kipindi kirefu, alitokea Mtibwa Sugar na baadaye alirejea katika timu hiyo kabla ya kurudi tena Simba.


Mgosi amesema wanaujua ubora wa Mtibwa, mechi itakuwa na ushindani lakini imani ni kubwa kuwa Simba itafanya vizuri kwa kuwa ina kikosi bora zaidi ya Mtibwa Sugar.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV