January 22, 2017
Simba imeanza vizuri hatua ya kuwania Kombe la Shirikisho kwa kuitwanga Polisi Dar es Salaam kwa mabao 2-0.

Polisi ilionyesha soka safi lakini ikashindwa kuhimili vishindo vya Simba, hadi mapumziko ilikuwa imefungwa kwa bao moja lililofungwa na Patory Athanas.

Kipindi cha pili, Simba waliingia na kasi lakini kipa wa Polisi Dar ndiye alikuwa shujaa kutokana na kuokoa michomo mingi ya hatari.

Laudit Mavugo na Shiza Kichuya, walipoteza nafasi nyingi kwa upande wa Simba huku wakishindwa kuutegua mtego wa offside wa Polisi mara kwa mara.


Dakika chache kabla ya filimbi ya mwisho, Mohamed Zimbwe Jr, aliifungia Simba bao la pili kwa kichwa baada ya shuti lake kugonga mwamba baada ya kuuvunja mtego wa kuotea wa Polisi. Halafu ukamkuta na kuupachika wavuni.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV