January 20, 2017


Shujaa wa Tanzania siku chache zilizopita, Alphonce Simbu amekutana na mshangao baada ya kutua jijini Dar es Salaam na kukuta hakuna mwenyeji hata mmoja aliyekwenda kumpokea kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JKIA).

Simbu amekuwa shujaa wa Tanzania baada ya kushinda Marathoni ya Mumbai nchini India akibeba medali ya dhahabu.

Pamoja na hivyo, alitua nchini na kwenda kwao Kanda ya Kaskazini. Lakini leo ndiyo ilikuwa siku aliyotakiwa kuja jijini Dar es Salaam.

Baada ya kukosa wenyeji zaidi ya waandishi wa habari waliofika uwanjani hapo, madereva taxi wa uwanjani hapo, waliamua kuchukua jukumu la kumpokea.

“Kama wamemuona hafai, basi sisi tutakuwa ni wenyeji wake,” alisema mmoja wa madereva hao, akamchukua na kwenda kumkabidhi kwa wenzake.

“Kaa hapa wakija tuwape vidonge vyao,” alisema akimuelekeza akae katika meza ambayo madereva hao hukaa wakisubiri wateja.

Simbu alikaa katika eneo hilo kwa muda wa zaidi ya dakika 40 akiwasubiri wenyeji wake ambao walichelewa sana.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV