January 20, 2017Mshambuliaji nyota wa zamani wa TP Mazembe, Thomas Ulimwengu amekiri kumalizana na AFC ya nchini Sweden.

Ulimwengu amesema anatarajia kuondoka nchini Jumapili kwenda nchini Sweden kumalizana na AFC inayoshiriki Ligi Kuu ya Sweden. 

Awali aliichezea AFC lakini timu ya vijana na timu hiyo ndiyo ilimuuza TP Mazembe alikofanya vizuri.

“Ndiyo, nakwenda Sweden Jumapili. Nitajiunga na AFC,” alisema Ulimwengu.

Kwa AFC ya nchini Sweden, Ulimwengu ni kama anarejea nyumbani kwa kuwa ndiyo timu yake ya kwanza kuichezea barani Ulaya,


Ulimwengu alijiunga na timu hiyo akitokea Tanzania baada ya kupelekwa na wakala wa kuuza wachezaji anayetambuliwa na Fifa wakati huo, Damas Daniel Ndumbaro.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV