January 15, 2017
TANZIA:
Uongozi wa klabu ya soka ya Yanga umepokea kwa mbadiliko  kifo cha kuumiza cha Mwandishi wake habari za michezo wa Gazeti la Uhuru Bi, Amina Athumani kilichotokea uko Zanzibar.

Marehemu Amina amefariki akiwa ametoka kutekeleza majukumu yake ya kazi kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi uko visiwani Zanzibar.

Amina licha ya kuwa mwandishi wa habari za michezo lakini pia Alikuwa mwanachama Wa  YANGA tawi la WhatsApp SUPPORTERS MAKAO MKUU.

Uongozi unaungana na familia ya marehemu, ndugu jamaa pamoja na tasnia nzima ya waandishi was habari nchini katika kuomboleza kifo chake.

Innaa Lillaahi wa innaa Ilayhi raaji'uun. 

Imetolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano Yanga Makao Makuu.

15/01/2017

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV