January 17, 2017


Klabu ya West Ham imeamua kumwaga mboga baada ya kukataa ofa ya pauni million 22 kutoka kwa klabu ya Marseille ya Ufaransa.

Marseille imetoa ofa hiyo ili kumpata kiungo Mfaransa  Dimitri Payet.

Hata hivyo West Ham imeweka msisitizo kwamba Payet hatakwenda popote Januari hii, maana yake haina mpango wa kumuuza.

Hii imetokea baada ya siku chache zilizopita Payet kugoma kufanya mazoezi akishinikiza kuuzwa hali iliyosababisha mashabiki kumzomea kila wanapomuona au kuziona picha zake.


Pamoja na West Ham kuweka msisitizo huo, Rais wa Marseille, Jacques-Henri Eyraud ametua jijini London kuangalia kama anaweza kulimaliza suala hilo kwa kuzungumza na bosi wa West Ham, David Sullivan.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV