January 26, 2017Yanga wameendelea kufanya mazoezi wakijiweka vizuri kwa ajili ya mechi yao ijayo ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Mwadui FC.

Yanga itashuka kuivaa Mwadui FC kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam huku ikiwa imejua matokeo kati ya mtani wake Simba dhidi ya Azam FC Jumamosi. Simba iko kileleni ikiizidi Yanga pointi mbili tu, kama itayumba na kupoteza au kupata sare dhidi ya Azam FC, Yanga itakuwa na kazi moja tu ya kuifunga Mwadui FC na kukaa kileleni.

Wachezaji wa Yanga wamekuwa wakiendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kujiandaa na mechi hiyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV