January 23, 2017Mabingwa wa Ligi Kuu Bara na Mabingwa wa Kombe la Shirikisho, Yanga wameendelea kujifua kuhakikisha wanatetea makombe yao yote mawili au 'warembo' wawili inaowashikilia.

Katika Ligi Kuu Bara, Yanga iko katika nafasi ya pili nyuma ya Simba lakini tayari wameanza michuano ya Kombe la Shirikisho kwa kuitwanga Ashanti kwa mabao 4-1, juzi.

Chini ya Kocha George Lwandamina, Yanga walifanya kazi ya kujifua kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV