March 17, 2017
Mtaalamu kutoka nchini China ndiye atakayeweka nyasi bandia kwenye Uwanja wa klabu ya Simba.

Mtaalamu huyo, atatumia siku tano tu kukamilisha kazi yake hiyo huko Bunju nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema bado wanahaha kuzikomboa nyasi bandia bandarini.


“Nafikiri tuko mwishoni, lakini tukifanikiwa basi ni jambo la siku tano tu,” alisema Hans Poppe.“Yule mtaalamu amesema siku tano lakinia tahitaji nguvu kazi ya ziada. Hapa tunaomba mvua zisiwe kubwa zikaharibu mambo maana tulishaanza.

“Kilichobaki ni suala la kutandika mabomba, leya ya mwisho halafu baada ya hapo ni nyasi.

“Lakini Kama mvua itaendelea kunyesha. Basi tutaingia hasara kubwa na kulazimika kuanza upya tena,” alisema Hans Poppe.


1 COMMENTS:

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV