June 30, 2017

Kumekuwa na mjadala unatembea mitandaoni kuhusiana na Haji Manara kuangua kilio mahakamani Kisutu, jana.

Manara ambaye ni msemaji wa Simba, aliangua kilio baada ya Rais wa Simba, Evans Aveva na makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ kutakiwa kwenda mahabusu baada ya kusomewa mashitaka ya utakatishaji fedha.Suala hilo lilionyesha kumuumiza Manara ambaye alitafuta sehemu akakaa na kuangua kilio hasa baada ya kusikia wanakwenda mahabusu hadi Julai 13, kesi yao itakaposikilizwa leo.

Katika makundi mbalimbali ya Whatsapp ambayo yanahusisha Yanga au Simba, wengi wamekuwa wakimuonea huruma Manara kutokana na picha zinazomuonyesha akiangua kilio.

Wengine wamekuwa wakimtania kutokana na utani wa Yanga na Simba lakini asilimia kubwa wakimpa moyo kutokana na matatizo yanayowakabiri.2 COMMENTS:

  1. Kinachomliza nini? Hajui takukuru wanasimamia maslahi ya Simba? Au naye anahusika? Atulie tu haki ifuate mkondo wake. Kama hawahusiki si watatoka? Unaweza lia halafu mwishoni ikathibitika walifanya ufisadi, tutakuweka kundi gani? Labda kama analilia rafiki zake tu

    ReplyDelete
  2. Kinachomliza nini? Hajui takukuru wanasimamia maslahi ya Simba? Au naye anahusika? Atulie tu haki ifuate mkondo wake. Kama hawahusiki si watatoka? Unaweza lia halafu mwishoni ikathibitika walifanya ufisadi, tutakuweka kundi gani? Labda kama analilia rafiki zake tu

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV