June 30, 2017
Beki king’ang’anizi wa Yanga, Hassan Kessy, amesikia majigambo ya Simba tangu wamrejeshe kiungo mshambuliaji Mganda, Emmanuel Okwi na kutamka: “Subirieni huyo mchezaji wenu kama atacheza mbele yangu.”

Simba ilifanikisha mipango ya kumsainisha mshambuliaji huyo hivi karibuni ikimsainisha mkataba wa miaka miwili ya kuichezea timu hiyo inayojiandaa na Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho.

Huyo, ni mchezaji wa nane kusajiliwa na Simba tangu usajili ufunguliwe Juni 15, mwaka huu na baadhi yao ni John Bocco, Shomari Kapombe, Jamal Mwambeleko na Aishi Manula. 

Kessy amesema siku zote anapenda akabane na mchezaji tegemeo wa timu pinzani kwa ajili ya kumpa ushindani ili aone upungufu wake na kuufanyia kazi.

Kessy alisema anaheshimu kiwango kikubwa alichonacho Okwi, lakini siyo kumuogopa na katika kuthibitisha hilo, ataanza kumuonyeshea kwenye mechi ya Ngao ya Jamii mara timu hizo zitakapokutana.

Aliongeza kuwa, uzuri wote wawili wanajuana aina ya uchezaji kutokana na kuwahi kukutana na mshambuliaji huyo yeye akiwa anaichezea Mtibwa Sugar na Okwi anaichezea Simba.

“Nimesikia majigambo wanayoyatoa Simba baada ya kumsainisha Okwi, niseme mimi sipendi kuongea, subirieni tutakapoonana uwanjani mimi nikiwa na Yanga na yeye Simba.

“Okwi siyo mchezaji mbaya, ni mzuri, ana uwezo mkubwa, lakini hatakiwi kupewa hizo sifa anazozipata kwa mashabiki wa timu hiyo.

“Kwa kifupi niseme kuwa tutaonana kwenye Ngao ya Jamii kabla ya kuanza ligi kuu halafu utaona kama wataongea tena,” alisema Kessy akiwa Afrika Kusini na timu ya taifa inayoshiriki michuano ya Cosafa.


2 COMMENTS:

  1. Chizi fresh, yeye mwenyewe pale yanga anasugua benchi, siku hio beki 2 ni Juma abdul sio yeye, km ana uwezo amuweke benchi Kapombe kule south.

    ReplyDelete
  2. Chizi fresh, yeye mwenyewe pale yanga anasugua benchi, siku hio beki 2 ni Juma abdul sio yeye, km ana uwezo amuweke benchi Kapombe kule south.

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV