June 26, 2017


Msimu uliopita kikosi cha Kagera Sugar kilikuwa na tatizo katika upande wa beki ya kushoto.

Kutokana na hali hiyo, uongozi wa klabu hiyo unadaiwa ulitua makao makuu ya Klabu ya Yanga na kuulizia kama Oscar Joshua bado ana mkataba na klabu hiyo.

Hata hivyo, baada ya kuambiwa kuwa mkataba wake umemalizika, uongozi huo  unadaiwa kuanza mchakato wa kuhakikisha unamsajili kwa ajili msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

Kuna taarifa taarifa Kagera umeanza mazungumzo na Joshua lakini mambo yamekuwa yakienda kwa siri kubwa kwa kuwa Yanga nao wameshindwa kuweka msimamo moja kwa moja.

Kumekuwa na taarifa Yanga inataka kumuacha Joshua lakini kutokana na kuzorota kiuchumi, imekuwa ikishindwa kufanya maamuzi kwa kuwa haina uhakika wa kufanya usajili mbadala.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV