June 29, 2017


Kiungo wa Everton, Morgan Schneiderlin ameendelea kula bata na sasa amehamia Zanzibar.

Schneiderlin yuko nchini na alianzia kula bata mbugani Serengeti na sasa yuko Zanzibar akiendelea kushikilia fungate na mkewe mpya. Vyombo vya habari Uingereza vimeendelea kumfuatilia huku vikieleza kuwa yuko nchini Tanzania.


 Schneiderlin atarejea nchini Julai 11 akiwa na Everton kuwavaa Gor Mahia Julai 13 ambao ni mabingwa wa SportPesa Super Cup.

Mechi hiyo itapigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na tayari inasubiriwa kwa hamu na watu.
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV