June 29, 2017

MALINZI ALIPOWASILI MAHAKAMANI KISUTU, LEO.

Rais wa TFF, Jamal Malinzi, katibu wa TFF, Mwesigwa Celestine na Nsiana wamesomewa mashtaka 28 katika mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya mashitaka hayo ni kughushi waraka wa kamati ya utendaji ulioonyesha kuwa imeridhia kubadilishwa kwa Signatories (watu wanaosaini nyaraka za benki kutoa fedha). Shitaka hilo linawahusu Malinzi na Mwesigwa.

Malinzi amedaiwa kugushi risiti za kwamba anaidai TFF na ziko risiti 20 ambazo anatuhumiwa kuzifoji.


Shitaka jingine ni utakatishaji na hii wote watatu, Malinzi, Mwesigwa na Nsian wanatuhumiwa kutakatisha kiasi cha dola 375418.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV