June 28, 2017
Mshambuliaji Henry Onyekuru amejitangaza kusajiliwa na Everton.

Mshambulizi huyo alikuwa anakipiga KAS Eupen ya Ubelgiji katika ligi inayoshiriki Genk anayoitumikia Mtanzania, Mbwana Samatta.

Onyekuru raia wa Nigeria amejitangaza kujiunga na Everton hata kabla ya klabu hiyo kumtangaza.

Kabla Onyekuru  alikuwa anawaniwa na Arsenal na West Ham, lakini picha aliyopiga mbele ya logo ya Everton inaonyesha ameishamalizana nayo.Everton itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Gor Mahia kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.


Mashabiki wamekuwa wakiisubiri kwa hamu mechi hiyo na kati ya wachezaji watakaoshuhudiwa na mashabiki wa soka nchini ni Onyekuru.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV