June 26, 2017Huku zoezi la usajili likiendelea kushika kasi katika timu mbalimbali zinazoshiriki ligi kuu, timu ya Yanga inadaiwa kutaka kumrejesha kiungo wake Salum Telela.

Telela ambaye awali aliwahi kuichezea Yanga kabla ya kwenda Ndanda ya Mtwara, anatarajiwa kurejeshwa kundini ili kuziba pengo la kiungo Haruna Niyonzima aliyeachana na timu hiyo.

Taarifa zinaeleza kwamba baada ya Yanga kuona kiungo wake Niyonzima ametimka, wameamua kumrejesha Telela ili aweze kuziba nafasi hiyo ambayo anaimudu kwa asilimia kubwa.

Kwa sasa kiungo huyo yupo katika mazungumzo na klabu yake hiyo ya zamani ili kuona uwezekano wa kusaini mkataba.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV