June 27, 2017

STAA wa Muziki wa Hip Hop Bongo, Ibrahim Musa ‘R.O.M.A Mkatoliki’ kwa mara ya kwanza ameweka historia katika Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar live baada ya kutua akiwa ndani ya ‘crane’ akitokea nje ya ukumbi.

Katika shoo hiyo iliyowakutanisha mastaa kibao wakiwemo Stamina, Mr. Blue, Snura, Darassa na Madee, Roma aliingia akiwa katika vazi jeupe na kupiga nyimbo zake kibao zikiwemo K, Viva Roma Viva, Tanzania na Usimsahau Mchizi.


Kivutio kingine kilichoteka ukumbini ni pale alipoingia na msanii mwenzake ambaye walitekwa naye hivi karibuni, Moni ambapo waliingia wakiwa wamefungwa vitambaa usoni mithili ya mtu aliyetekwa.
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV