June 26, 2017Uongozi wa Ruvu Shooting ya Pwani umefunguka kuwa, upo katika mazungumzo mazuri ya kumuongeza mkataba kiungo wake Shabani Kisiga kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo katika msimu ujao wa ligi kuu.

Kisiga ambaye aliichezea Ruvu Shooting msimu uliopita, amemaliza mkataba wa kuitumikia timu yake hiyo.

Msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire, alisema kuwa wapo katika mazungumzo mazuri na kiungo huyo na kudai kuwa pande zote mbili zinaonyesha kuhitajiana.

“Sisi tunampenda Kisiga aweze kuendelea kuichezea timu yetu na kwa upande wake pia inaonyesha anapenda kuendelea na sisi hivyo wote tunapendana.


“Tunaendelea na mazungumzo na iwapo yatakamilika basi wakati wowote ataongeza mkataba mwingine,” alisema Masau.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV