June 27, 2017
Kiungo wa pembeni wa Azam FC, Ramadhani Singano amefuzu vipimo vya afya vya klabu ya Difaa Al Jadida ya Morocco.

Difaa Al Jadida ilimtumia mwakilishi wake nchini kumfanyia Singano maarufu kama Messi vipimo vya afya na taarifa zimeeleza kuwa amefuzu.

"Sasa ni suala la viza tu, kama hili likikamilika, basi Singano ataondoka. Hawataingia naye mkataba sasa hivi hadi mkataba wake na Azam FC utakapoisha siku chache zijazo.

"Ila kuna taarifa nimeambiwa wamemtaka kwenda kule mapema ili kuzoea mazingira," kilieleza chanzo.

Mkataba wa Singano na Azam FC umebakiza siku chache kwisha na hivi karibuni ilielezwa mchezaji huyo kugoma kusaini mkataba mpya Azam FC
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV