June 26, 2017


Leo ni sikukuu tukufu ya Iddi, ninaamini kila mmoja wetu ana haki ya kufurahia.

Lakini litakuwa nina ujumbe kwako, kwamba hakikisha unasherekea sikukuu yako bila ya vurugu wala ugomvi. Usitaka kumkwaza mtu au kumsababishia matatizo.

Jitahidi kuwa na nidhamu na uonyeshe Watanzania ni watu wanaojitambua, wenye upendo na kila mmoja afurahi kwa raha zake na familia yake, rafiki na jamaa zake.

Askari wanaolinda kila sehemu nao ni wanadamu, pia wana haki ya kusherekea, tuwapunguzie kazi ya kutulinda wakati hata sisi tunaweza kujilinda kama tunajitambua.

Kila jambo hupangwa na Mwenyezi Mungu, lakini kuhusiana na kuonyesha upendo, ni ndani ya uwezo wa mwanadamu, mimi na wewe.


NIKUTAKIE IDDI NJEMA YENYE AMANI NA UPENDO.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV