June 27, 2017


Mchezaji wa Oklahoma City Thunder, Russell Westbrook ndiye mchezaji bora wa NBA kwa msimu wa 2016-17.

Pamoja na kwamba bingwa ameibuka kuwa Golden State Worriers lakini Westbrook ndiye amoeba tuzo ya jumla kuwa mchezaji bora wa NBA.
Katika miaka 55, Westbrook amekuwa mchezaji wa pili kuwa wastani wa triple-double kwa msimu mzima.

Ameshinda tuzo hiyo akiwa ameshinda kutoka Houston Rockets James Harden na Kawhi Leonard wa San Antonio Spurs alioingia nao fainali.
Westbrook alipata wasyani wa mind-boggling 31.6, asisti 10.4 kwa mechi na  ribaundi 10.7.
Wastani huo wa juu kabisa ni katika mechi 81 alizocheza za msimu uliopita.

Mara ya mwisho mchezaji aliyefikia viwango via juu kama vyake ilikuwa ni katika msimu wa 1961-62 wa NBA na alikuwa ni Oscar Robertson.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV