June 28, 2017

KOMBA


Wakili wa viongozi wa juu wa TFF, Alloyce Komba amesema hajui makosa ambayo wateja wake wameshikiliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Komba amesema hadi sasa hajui Rais wa TFF, Jamal Malinzi na Katibu Mkuu TFF, Mwesigwa Celestine wanashikiliwa kwa sababu zipi.

“Hadi sasa sijui wameshikiliwa kwa sababu zipi, Takukuru hawajasema lolote.

“Mimi ni wakili wao, sijui lolote hadi sasa jambo ambalo si sahihi,” alisema.

Komba ambaye ni mwandishi kitaaluma amesema lingekuwa jambo jema kama Malinzi na Mwesigwa wangeachiwa na Takukuru kwa dhamana.

Taarifa za awali zilieleza kuwa Malinzi na Mwesigwa walikuwa wakigojiwa kwa matumizi mabaya ya ofisi na utakatishaji fedha.

Baadaye leo mchana, Takukuru walikiri kuwashikilia lakini pia hawakutaka kufafanua wanahojiwa kwa makosa yapi.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV